Wednesday, September 28, 2022
No menu items!
HomeYour CountyBungomaMbunge was Kanduyi Wafula Wamunyinyi aonyeshwa mlango

Mbunge was Kanduyi Wafula Wamunyinyi aonyeshwa mlango

 

Eneo bunge la Kanduyi ambalo ndilo eneo bunge kubwa zaidi kaunti ya Bungoma likiwa na wapiga kura 118,333 limepata mbunge mpya.

 

Matokeo yametangazwa na afisa mkuu wa IEBC eneo bunge hilo Stanley Kipkosgei mnamo Alhamisi asubuhi.

 

Wakili John Makali wa Ford Kenya alikusanya kura 32,099 huku kinara wa DAP-K Wafula Wamunyinyi akizoa kura 20,240. Alfred Khang’ati wa chama cha ODM alikuwa wa tatu kwa kura 12,970. 

 

Wawakilishi wadi waliojishindia kura hizo ni kama wafwatavyo. George Makari, Ford Kenya alishinda Evans Wasike , DAP K, huko Musikoma kwa kura 2,731 huku Evans akipata kura 2180.

Peter Wanjala , Ford Kenya, alishinda uwakilishi wadi wa Bukembe Mashariki kwa kura 3,284 naye Joram Wanjala , DAP K akizoa kura 2,389 katika kinyang’anyiro hicho.

        

Bukembe Magharibi kulishudiwa kivumbi kikali baina ya Anthony Lusenaka wa DAP K ,Briver Simiyu UDA, na Richard Jesome wa Ford K ambapo Lusenaka aliwabwaga wapinzani wake kwa kura 2,185 huku Jesome na Simiyu wakizoa kura 1,864 na 1,839 mtawalia.

        

Cornelius Wanjala , DAP K alikiwahi kiti cha uwakilishi wadi wa Khalaba kwa kura 2,883 huku mpinzani wake Okumu Henry Majimbo , Ford K akinyakua kura 2008.

       

Evertone Sifuna, (DAP K) alishinda kule Sang’alo Mashariki kwa kura 2,820 akifwatwa na Simon Wafula, Ford K aliyezoa kura 2,355.

       

Mukhwana Godfrey Wanyama , Independent, aliwapiku wapinzani wake kule Sang’alo Magharibi kwa kuzoa kura 3,873 huku Wesonga Musebe, Ford K akipata 1,376.

       

Kule Tuti Marakaru, Nyongesa Joseph , Ford K, aliwawahi wapinzani kwa kuwabwaga mapema asubuhi akijizolea kura 4,502 naye mpinzani wake wa karibu Beatrice Nekesa , DAP K, akifanisi kura 1,502 pekee.

      

Jeremiah Kulobah , DAP K alipata kura 2,506 katika mapambano ya wadi ya Township naye Kassim Ayub , UDA, akipata kura 2,139.

      

Mwenyekiti wa IEBC tawi la Bungoma Bi. Grace Rono ameongea na KNA na kuahidi kuwa matokeo ya jimbo nzima yatatangazwa leo kabla ya saa mbili usiku.           

 

       

Source:KNA

 

The Countyhttps://thecounty.co.ke
The County brings you comprehensive and unrivaled coverage of the happenings in all 47 Kenyan counties. It has not happened in mashinani if it is not on The County!
RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -

Most Popular