Gavana wa kaunti ya Makueni Kivutha Kibwana amewahimiza viongozi na wananchi wa kaunti hiyo kuandaae kampeni za amani wakati huu tumekaribia uchaguzi mukuu.
Akizungumza siku ya jumapili kwenye kanisa la kotoliki la Mtakatifu Joseph the worker mjini Wote Kaunti ya Makueni, kwenye hafla ya kumuaga Padri wa parokia hiyo Paul Munguti ambaye alipata uhamisho, Kibwana amewataka viongozi na wananchi kudumisha amani na usalama wakati na baada ya uchaguzi.
Munguti ambaye amehudumu kwenye Parokia ya Makueni Kwa zaidi ya Miaka kumi alipata uhamisho kwenda kufanya kazi kwenye shule ya upili ya kimishonari Katoloni.
“Ni jukumu la Kila kiongozi na mwananchi kudumisha amani na usalama wakati huu tunapokarabia uchaguzi mkuu,” Kivutha alisema.
Wito huo unakuja ikiwa zimesalia takriban siku thelathini na tano kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Gavana Kibwana pia aliwataka viongozi ambao wanaeneza siasa za matusi kwa wapinzani wao kukoma na kuuza sera Kwa Wananchi badala yake.
“Watu wafanye siasa za sera badala ya matusi na kueneza propaganda,” aliongezea.
Wakati huo huo Mbunge wa Makueni Daniel Maanzo na ambaye anamezea mate kiti cha useneta Kaunti ya Makueni akizungumza kwenye hafla hiyo amewataka viongozi wa kidini kuwarai wananchi kujitokeza kupiga kura maana ni wajibu wao kama wapiga kura, ili kuweza kuwachagua viongozi bora watakaoimarisha hali ya uchumi nchini.
“viongozi wa kanisa ni wajibu wenu kuhimiza wananchi kujitokeza kupiga kura ili wapate kuchagua viongozi bora,” Maanzo alisema.
Amewaomba kuwa mstari wa mbele kupigana na ufisadi kupitia shule ambazo zinamilikiwa na kanisa Kwa kuweka maadili mema Kwa wanafunzi.
Alisema kuwa ni kupitia shule za kidini wanafunzi wanaweza kupata maadili ya uongozi wakiwa wachanga, maadili ambayo yatasaidia kukuza viongozi wa kesho wasio wafisadi.
“Tuweke maadili mema Kwa wanafunzi kupitia shule zetu ambazo tunazimiliki kama kanisa hili waweze kujua kuwa kupora Mali ya umma ni jambo mbaya na ambalo halistahili kamwe,” Maanzo alisema.
Viongozi wengine walioudhuria hafla hiyo ni Mwakilishi wa wadi ya Makueni(MCA) Felix Mateso na David Masika ambaye anagombea kiti cha ugavana kaunti ya Makueni.
Viongozi hao wamemsifu Padri Munguti Kwa kazi nzuri ambayo amefanya kwenye Parokia ya Makueni Kwa hiyo miaka yote amekuwa kwenye Parokia hiyo na kumutakia Kila la heri kwenye kazi anayoenda kufanya Katoloni.
Source:KNA